Dira ya Halmashauri ya Manispaa ni kuwa moja kati ya Halmashauri bora nchini yenye uwezo mzuri wa kutoa huduma bora na endelevu kwa wadau wake wote ifikapo mwaka 2025
Maono ya Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ni kuongeza uwezo wa jamii mchanganyiko katika kuendeleza utawala bora, ukuaji wa uchumi, maisha bora na mazingira endelevu.
MALENGO
Lengo Kuu
Lengo kuu la Halmashauri ya Manispaa katika kuandaa mpango mkakati wake ni kuhakikisha maisha bora ya wananchi wa Manispaa ya Lindi kwa kutoa huduma bora zaidi za jamii ili kupanua wigo katika kuvutia uwekezaji wa sekta mbalimbali zilizopo Manispaa ya Lindi.
MALENGO MAHUSUSI
Ili kufanikisha lengo kuu, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi imejiwekea malengo mahususi kama ifuatavyo:-
Kuboresha huduma za jamii na kupunguza maambukizi mapya ya VVU
Kuendeleza utekelezaji wa mkakati wa taifa wa kupambana na kuzuia rushwa
Kuboresha na kuongeza upatikanaji wa huduma za jamii
Kuimarisha utawala bora na huduma za kiutumishi
Kuboresha utayari wa kukabiliana na matukio na majanga
Kuongeza kiwango na ubora wa huduma na miundombinu ya kiuchumi
Miundombinu ya kiuchumi ni kigezo muhimu katika ukuaji wa uchumi na maendeleo katika uchumi wowote duniani. Halmashauri inalazimika kuboresha huduma na miundombinu ya kiuchumi ili kukuza uchumi wa wananchi wa Manispaa ya Lindi kwa kutumia vizuri rasilimali zake zilizopo. Ukuaji wa uzalishaji katika kilimo na mifugo, uvuvi, maliasiri, biashara na viwanda itasababisha mabadiliko katika kiwango cha ukuaji wa uchumi wa Manispaa ya Lindi.
Kuboresha usimamizi wa maliasiri na mazingira
Halmashauri ya Manispaa ya Lindi inaamini kuwa popote pale duniani, uchumi endelevu hutegemeana na usimamizi na uhifadhi endelevu wa mazingira. Ukuaji wa uchumi hutegemea mazingira yake, hivyo Halmashauri itahakikisha usimamizi mzuri wa mazingira ya rasilimali na maliasiri zilizopo na kuboresha usafi na mazingira.
Kuboresha mipango shirikishi, ufuatiliaji na tathmini ya miradi
Mzunguko wa mipango kuanzia ngazi ya chini ni njia inayotumika katika kuweka mipango na bajeti ya Serikali za Mitaa. Halmashauri ya Manispaa itahakikisha jamii inashiriki kikamilifu katika kuibua na kuweka mipango ya maendeleo. Ufuatiliaji na tathmini nzuri ya miradi ni nguzo ya utekelezaji mzuri wa miradi na Halmashauri itahakikisha ufuatiliaji unafanyika kikamilifu na kwa ufanisi.
Kutokana na malengo mahususi ya Halmashauri yaliyojadiliwa hapo juu, kila sekta/idara katika Halmashauri ya Manispaa imeweka malengo ya utekelezaji wake ili kufanikisha lengo kuu la Halmashauri. Kila sekta/idara itakuwa na malengo yake bila kuingiliana kati ya idara na idara ili kuongeza uwajibikaji. Hivyo idara zimejiwekea malengo ambayo yameainishwa katika sura ya nne kwa utekelezaji wa lengo kuu la Halmashauri.
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255767042958
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa