Ili kupata leseni ya Biashara unatakiwa kufanya yafuatayo:-
KWA MUOMBAJI MPYA
1. Fika ofisi za Biashara za Halmashauri kwa Afisa Biashara utajaza fomu ya kuomba leseni.
2. Utapewa maelekezo ya kwenda TRA kwa ajili ya kupata TIN namba na kufanya Tax Clearance
3. Ukishapata TIN utarudi tena kwa Afisa Biashara ukiwa na kopi ya TIN yako na utatengenezewa Bill ambayo utaenda nayo NMB kwa ajili ya kufanya malipo
4. Mara baada ya kulipa utarudisha nyaraka kwa mpokea fedha wa Halmashauri na kupewa Risiti ya Halmashauri
5. Rejesha risiti kwa Afisa Biashara ambapo yeye atakupatia Leseni yako ikiwa imekamilika.
KWA WANAOHUISHA LESENI ZAO
1. Nenda TRA kwa ajili ya kufanya Tax Clearance
2. Fika Ofisi za Biashara ukiwa na leseni yako ya zamani ili utendengenezewe Bill ili uende kulipia NMB
3. Mara baada ya kulipa utarudisha nyaraka kwa mpokea fedha wa Halmashauri na kupewa Risiti ya Halmashauri
4. Rejesha risiti kwa Afisa Biashara ambapo yeye atakupatia Leseni yako ikiwa imekamilika.
NB:
Unaweza kulipia Bill yako kwa kutumia huduma ya NMB Mobile kwa wateja wenye huduma hiyo Kupitia hatua zifuatazo:-
1. Piga *150*66#
2. Ingiza Password
3. Chagua 5 - Malipo ya Bill
4. Chagua 8 - TAMISEMI
5. Chagua 2 - Lipia Bill
6. Ingiza namba ya malipo ambayo ni ndefu inaanzia na 2006.......
7. Itakuonesha Jina la Mteja na Deni lake
8. Chagua kulipia bill
9. Thibitisha Malipo.
Mkurugenzi wa Manispaa
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255767042958
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2018 Manispaa ya Lindi. Haki Zote Zimehifadhiwa