Halmashauri ya Manispaa inapenda kuona kuwa dira yake inafikiwa kikamilifu. Ili kufanikisha hilo, masuala muhimu yafuatayo yametazamwa kwa makini wakati wa maandalizi ya dira na malengo yake:-
Utawala bora
Kuimarisha amani na kutii sheria hutegemea sana suala la utawala bora katika utendaji kazi wa menejimenti ya manispaa na watumishi wake wote. Watumishi wote watazingatia kanuni na taratibu za utumishi wa umma katika kutekeleza majukumu yao. Hivyo ni vema kusema kuwa kutokuwepo kwa matabaka na kufanya maamuzi kwa wakati ni nguzo muhimu katika kufanikisha masuala ya utawala bora katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
Utoaji wa huduma bora
Menejimenti na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi watatoa huduma zilizo bora kwa kuzingatia na kutambua mahitaji muhimu ya makundi yote ya wananchi wa Manispaa bila kubagua kundi Fulani.
Uwazi na Uwajibikaji
Menejimenti itawajibika kutoa huduma kwa kujituma kufuatana na ujuzi na uzoefu wake katika kuwahudumia wananchi.
Mipango shirikishi
Kazi za Halmashauri ya Manispaa ya Lindi lazima zifanyike kwa usawa na hatua zote zizingatie uwazi na kuhakikisha wananchi na wadau wote wengine wanashiriki katika mipango ya Halmashauri ili kuboresha hali ya mipango na utekelezaji wake. Hili ni sual la muhimu lililozingatiwa katika kuweka dira ya HAlmashauri.
Uchumi endelevu
Kuhakikisha kuwa na uchumi endelevu ni jambo muhimu la kuzingatia katika kuweka dira na malengo ya Halmashauri. Hii ni matokeo ya mwisho katika utekelezaji timilifu wa malengo ya Halmashauri katika kufanikisha dira yake. Maendeleo yaliyo endelevu huonyeshwa na uchumi endelevu katika kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa na huduma.
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255767042958
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa