![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
Mkuu wa wilaya wa lindi amekabidhi Ambulance Mpya katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa sokoine huku akiwataka wauguzi na Madkatri kutumia Ambulance hiyo kuwafikia Wananchi kwa wakati pale wanapopatwa na Matatizo au Wanapohitaji huduma ya Ambulance hiyo kuwapeleka katika maeneo Mengine hususani Rufaa ya Nje ya Mkoa.
Akizungumza katika hafla ya Kukabidhi Ambulance hiyo ambayo Imetoka Wizara ya Afya kushirikiana na GLOBAL FUND "Tumekabidhiwa Ambulance Mpya, Serikali inaendelea kufikisha huduma za Afya kwa wananchi wake wa hali zote , Tuitunze Gari hii Maana itatusaidia kupunguza Vifo ambavyo vinatokea kwa kushindwa kusafirisha Mgonjwa kwa Wakati, Pia Bodi ya ushauri wa Hospitali hii Hakikisheni Mnakuwa na Mpango mkakati katika utoaji huduma kwa wananchi na tuwafikie wale walio mbali na maeneo ya kutoa huduma"
Ambulance hiyo pia ni kama Zahanati ndogo ikiwa na sheheni ya vifaa na huduma ya kwanza kwa Wagonjwa ambao watakuwa wanaopata huduma Kipindi wanaelekea Kituo cha Afya.
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255767042958
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa