![]() |
![]() |
![]() |
Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Ndugu Jomaary Satura akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga wamekabidhi pikipiki nane(8) aina ya Honda kwa maafisa Kilimo na ugani nane kutoka kwenye jimbo la Mchinga.
Akizungumza katika tukio hilo Mkuu wa Wilaya Mhe. Shaibu Ndemanga amesema "Pikipiki hizi mmekabidhiwa ili muwafikie wananchi kwa wakati, ili muweze kuwatatulia changamoto zao. Wakati wa kupambana kwa nguvu zote umewadia ".
Pia, Mhe. Ndemanga alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa kwa kuwekeza nguvu zake kuwasaidia wananchi na kuwa karibu nao katika kutatua kero mbalimbali.
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255767042958
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa