Vijana 120 wafuzu mafunzo ya kilimo cha Kitalu Nyumba (greenhouse) kati ya tarehe 16/6/ na 27/6/2019.
Ofisi ya waziri Mkuu,Kazi,Vijana na wenye ulemavu imewezesha mafunzo ya kilimo cha kisasa, kilimo cha kitalu nyumba katika eneo la nanenane ndani ya viwanja vya maonesho Ngongo. Vijana 120 kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya Lindi wamenufaika na mafunzo haya na kujipatia ujuzi wa kutosha wa kutumia teknolojia hii kuongeza kipato.
.
Mafunzo haya yaliyotolewa na Seguco-Sokoine University Graduate Enterpreneurs Coorperative, wahitimu wa chuo Kikuu cha Kilimo Cha Sokoine.
Mafunzo haya yaliendeshwa kwa awamu mbili, awamu ya kwanza ikiwa ni namna ya ujengaji wa kitalu nyumba imara,kuweka miundombinu ya umwagiliaji kwa ajili ya kilimo. hii ilikuwa ni Kuanzia tarehe 10-15/6/2019. Mafunzo ya kujenga kitalu yalitolewa kwa vijana 20 (wanaume 13 na wanawake 7).
Awamu ya pili ya mafunzo ilihusisha kilimo chenyewe katika kitalu chumba.ikihusisha uandaaji wa udongo,uchaguzi wa mbegu bora nk. hii likuwa kwa kipindi cha kuanzia tarehe 16 hadi 27 Juni 2019. Mafunzo ya kilimo kwa kitalu nyumba jumla vijana 120, wanawake 63,wanaume 57 yalitolewa. walijitokeza. lengo la awali la mfadhili wa mafunzo ambae ni ofisi ya waziri mkuu,kazi,vijana na wenye ulemavu ilikuwa ni kutoa ufadhili kwa vijana 100 pekee.lakini mwitikio wa jamii ulikuwa mkubwa kiasi cha kwamba vijana 20 zaidi waliongezeka hawa walifadhiliwa na Mkurugenzi wa Manispaa ili wasipitwe na fursa hio muhimu.
Mkurugenzi wa Manispaa
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255767042958
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2018 Manispaa ya Lindi. Haki Zote Zimehifadhiwa