Katika siku ya nne na ya mwisho ya ziara yake mkoani Lindi, Mhe. Naibu Waziri OR-TAMISEMI amefanya ziara katika Manispaa ya Lindi.Akiwa Manispaa ya Lindi, Mhe. Naibu Waziri amekagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya shule mbili, ukarabati wa shule kongwe ya Sekondari Lindi, kukagua karakana ya utengenezaji samani za shule iliyomilikiwa na Manispaa ya Lindi, na kukagua mradi wa mabasi unaomilikiwa na kikundi cha vijana kilichonufaika na mkopo kutokana na mapato ya ndani (10% ya mapato ya ndani).Mhe. Naibu Waziri amepongeza kazi kubwa na nzuri iliyofanyika katika kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati kama ilivuyoelekezwa na thamani ya fedha iliyotumika inaonekana.
Aidha, Mhe .Naibu Waziri amezielekeza Halmashauri zote nchini kuiga ubunifu mzuri uliotumika katika Manispaa ya Lindi kwa kuanzisha karakana (viwanda vidogo) kwa ajili ya kutatua changamoto ya samani za shule ikiwemo viti na meza.
Naibu Waziri wa elimu OR-TAMISEMI akisikiliza maelezo ya utendajikazi wa karakana iliyobuniwa na Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
Mhe. Naibu Waziri amemaliza ziara yake Mkoani Lindi na kuelekea Mtwara.
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255767042958
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa