Mtandao wa barabara katika Manispaa ya Lindi ni wa uhakika na unapitika kipindi chote cha mwaka. Usafirishaji wa mazao ya chakula na bidhaa nyingine hadi kulifikia soko ni wa uhakika. Halmashauri ya Manispaa inaendelea kuboresha mtandao wa barabara kwa kufungua barabara zingine katika maeneo ya nje na mji ili kurahisisha zaidi usafirishaji wa mazao ya kilimo. Kwa sasa changamoto iliyopo katika sekta ya usafirishaji wa bidhaa kutoka Dar es salaam hadi Lindi kwa njia ya barabara inaendelea kupatiwa ufumbuzi baada ya muda mfupi ujao inategemewa kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo ambayo huleta usumbufu msimu wa mvua. Ni mategemeo ya Halmashauri kuwa baada ya kumalizika kwa ujenzi wa barabara hiyo itakuwa fursa kubwa kwa Halmashauri kutanua mtandao wa soko la wafanyabiashara kutoka Mikoa mingine ambapo itarahisisha zaidi upatikanaji wa bidhaa na kuongeza mzunguko wa pesa katika Manispaa ya Lindi. Hadi sasa Halmashauri ina mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 518.80 na ni mategemeo ya Halmashauri kuweza kuongeza urefu huo mara mbili zaidi.
Mkurugenzi wa Manispaa
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255767042958
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2018 Manispaa ya Lindi. Haki Zote Zimehifadhiwa