• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

Dira na Dhamira

DIRA

Dira ya Halmashauri ya Manispaa ni kuwa moja kati ya Halmashauri bora nchini yenye uwezo mzuri wa kutoa huduma bora na endelevu kwa wadau wake wote ifikapo mwaka 2025

MAONO

Maono ya Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ni kuongeza uwezo wa jamii mchanganyiko katika kuendeleza utawala bora, ukuaji wa uchumi, maisha bora na mazingira endelevu.

MALENGO

Lengo Kuu

Lengo kuu la Halmashauri ya Manispaa katika kuandaa mpango mkakati wake ni kuhakikisha maisha bora ya wananchi wa Manispaa ya Lindi kwa kutoa huduma bora zaidi za jamii ili kupanua wigo katika kuvutia uwekezaji wa sekta mbalimbali zilizopo Manispaa ya Lindi.

MALENGO MAHUSUSI

Ili kufanikisha lengo kuu, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi imejiwekea malengo mahususi kama ifuatavyo:-

Kuboresha huduma za jamii na kupunguza maambukizi mapya ya VVU

  • Kiwango ya maambukizi ya virusi vya ukimwi katika Manispaa ya Lindi ni asilimia 5.9 na kundi kubwa lililoathirika ni la umri kati ya miaka 18 na 45. Hili ni kundi muhimu katika uendeshaji wa shughuli za kiuchumi katika jamii ya Manispaa ambalo huathiri nguvu kazi. Hivyo mpango mkakati wa Halmashauri utazingatia shughuli za kupambana na kupunguza maambukizi mapya ili kuokoa maisha ya wananchi.

Kuendeleza utekelezaji wa mkakati wa taifa wa kupambana na kuzuia rushwa 

  • Rushwa ni suala linaloendelea kukua katika taasisi mbalimbali nchini. Rushwa hupunguza kiwango cha uwajibikaji na uwazi katika utendaji kazi. Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kama taasisi ya Serikali jukumu lake kuu ni kutoa huduma za jamii katika eneo lake la utawala katika njia zilizo halali na za kisheria. Halmashauri itahamasisha jamii katika kupinga na kutokomeza rushwa na kuhakikisha utawala bora.

Kuboresha na kuongeza upatikanaji wa huduma za jamii

  • Halmashauri huwajibika kutoa huduma za jamii zilizo bora na kuhakikisha zinapatikana kwa wananchi wake. Mpango mkakati huu utahakikisha unatolea ufumbuzi wa masuala nyeti katika huduma za jamii ili kufanikisha lengo kuu.

Kuimarisha utawala bora na huduma za kiutumishi

  • Utawala bora ni suala muhimu katika mafanikio ya jamii yoyote ile kwa kuwa huhusika katika kutoa maamuzi, utawala wa sheria, usimamizi wa rasilimali watu, uwazi, uwajibikaji, ufanisi, ufasaha, usawa na jinsia. Halmashauri ya Manispaa itatekeleza mpango mkakati wake kwa kuzingatia taratibu na kanuni za utawala bora ili kufanikisha mahitaji ya wananchi wake waliopo na wajao.

Kuboresha utayari wa kukabiliana na matukio na majanga

  • Utayari wa usimamizi wa matukio na majanga ni muhimu sana kwa Halmashauri katika kupunguza gharama zinazojitokeza wakati wa majanga yanapotokea kama moto, magonjwa ya mlipuko na maporomoko ya ardhi.

Kuongeza kiwango na ubora wa huduma na miundombinu ya kiuchumi

Miundombinu ya kiuchumi ni kigezo muhimu katika ukuaji wa uchumi na maendeleo katika uchumi wowote duniani. Halmashauri inalazimika kuboresha huduma na miundombinu ya kiuchumi ili kukuza uchumi wa wananchi wa Manispaa ya Lindi kwa kutumia vizuri rasilimali zake zilizopo. Ukuaji wa uzalishaji katika kilimo na mifugo, uvuvi, maliasiri, biashara na viwanda itasababisha mabadiliko katika kiwango cha ukuaji wa uchumi wa Manispaa ya Lindi.

Kuboresha usimamizi wa maliasiri na mazingira

Halmashauri ya Manispaa ya Lindi inaamini kuwa popote pale duniani, uchumi endelevu hutegemeana na usimamizi na uhifadhi endelevu wa mazingira. Ukuaji wa uchumi hutegemea mazingira yake, hivyo Halmashauri itahakikisha usimamizi mzuri wa mazingira ya rasilimali na maliasiri zilizopo na kuboresha usafi na mazingira.

Kuboresha mipango shirikishi, ufuatiliaji na tathmini ya miradi

Mzunguko wa mipango kuanzia ngazi ya chini ni njia inayotumika katika kuweka mipango na bajeti ya Serikali za Mitaa. Halmashauri ya Manispaa itahakikisha jamii inashiriki kikamilifu katika kuibua na kuweka mipango ya maendeleo. Ufuatiliaji na tathmini nzuri ya miradi ni nguzo ya utekelezaji mzuri wa miradi na Halmashauri itahakikisha ufuatiliaji unafanyika kikamilifu na kwa ufanisi.

Kutokana na malengo mahususi ya Halmashauri yaliyojadiliwa hapo juu, kila sekta/idara katika Halmashauri ya Manispaa imeweka malengo ya utekelezaji wake ili kufanikisha lengo kuu la Halmashauri. Kila sekta/idara itakuwa na malengo yake bila kuingiliana kati ya idara na idara ili kuongeza uwajibikaji. Hivyo idara zimejiwekea malengo ambayo yameainishwa katika sura ya nne kwa utekelezaji wa lengo kuu la Halmashauri.

Matangazo

  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA JANUARI 2023 December 15, 2022
  • Tangazo kwa umma: Uuzaji wa dawa muhimu kwa binadamu November 30, 2022
  • Kuitwa kwenye usaili November 08, 2022
  • TAARIFA KWA UMMA: MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI October 03, 2022
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LAAC YAPONGEZA UONGOZI NA WALIMU WA SHULE YA SEKONDARI LINDI PAMOJA NA KUTOA MAELEKEZO KWA TAMISEMI

    March 23, 2023
  • SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NI SIKU YA KUJIKUMBUSHA WAJIBU PAMOJA NA MAJUKUMU YETU . RC-TELACK

    March 08, 2023
  • MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE MANISPAA YA LINDI YAFANA.

    March 06, 2023
  • MANISPAA YA LINDI YAPOKEA PIKIPIKI 22 KUTOKA KWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KWAAJILI YA MAAFISA KILIMO

    March 13, 2023
  • Ona Yote

Video

Tamko la Mkuu wa Wilaya ya Lindi kuhusu zahanati ya Mnali
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa