Halmashauri 4 zanufaika na Shilingi Bil. 4.1 za kupanga,kupima na kumilikisha ardhi.
Asila Twaha , OR – TAMISEMI
Serikali imetoa kiasi cha shilingi billion 4.1 kwa Halmashauri nne zilizokidhi vigezo kuendeleza programu ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi nchini.
Hafla ya utiaji wa saini wa mikataba ya fedha umefanyika Juni 10, 2022 Jijini Dodoma.
Halmashauri zilizokidhi Vigezo hivyo ni Manispaa ya Kigamboni, Halmashauri ya Wilaya Kishapu, Manispaa ya Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa(afya)Dkt. Grace Magembe amesema, fedha hizi ni muendelezo wa awamu ya pili kwa Serikali kuzitoa kwa Halmashauri lengo likiwa Halmashauri kuzitumia kama ambavyo zilivyoelekezwa katika mikataba.
Amesema Halmashauri nyingi bado kuna changamoto ya ardhi kwa kutokupangwa na hii hupelekea kutokea kwa migogoro kati ya wananchi na Halmashauri kitu kinachosababisha kuzorotesha ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
“Ardhi ikipimwa wananchi wakijenga
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255717469888
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa