Mkuu wa Wilaya Ndugu Shaibu Ndemanga amepiga marufuku uongozi wa jumuiya za watumia maji kutumia pesa za miradi hiyo kwa matumizi binafsi au nje ya miradi ya maji kwani ni nje ya utaratibu wa kisheria lakini pia inapelekea kufa kwa miradi hiyo na kuifanya isiwe endelevu.Ameyasema hayo alipokuwa kwenye kikao kazi cha nusu mwaka kwa Vyombo vya watoa huduma ya maji wilaya ya lindi kilichofanyika leo tarehe 27/10/2021 katika ukumbi wa zamani wa lindi dc.
Vilevile Ndemanga amemuomba meneja wa RUWASA wa wilaya awe anampa mapato na matumizi kwa kila jumuiya wa watumia maji lakini pia kutoa taarifa ya upotevu wa vifaa vya miundo mbinu ya maji ili kupata picha ya kila jumuiya inakwendaje.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka jumuiya ya watumia maji kuhakikisha wanafanya kazi kulingana na taratibu lakini pia kutoa taarifa ya mapato na matumizi kwa wananchi kwani kutokutoa taarifa hizo hupelekea migogoro isiyo na sababu baina ya wananchi na uongozi.
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255717469888
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa