Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Zainab amesisitiza wazazi kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanaripoti shuleni ifikapo January 17/2022. RC Amesema “Watoto walikuwa wanabanana kwenye madarasa huko lakini Mhe. Rais akasema nataka watoto wasibanane lakini wasome vizuri waweze kufaulu vizuri ameleta fedha hizo ni nyingi Mkoa wetu pekeake tumepokea bilioni 8 na point. Kwahiyo niwaombe sasa wazazi tumejenga madarasa tumekamilisha tumetengeneza madarasa mazuri January watoto wanakuja kusoma naomba watoto wote watakaochaguliwa waje wakasome na kila mzazi naomba akawe mlinzi na mzazi mwenzie”. RC ametaka pia watoto walioolewa warudishwe nyumbani ili wakasome.
Ameyasema hayo leo alipokuwa akikabidhiwa madarasa 56 yaliyojengwa kwa pesa za mkopo kutoka IMF kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa UVIKO-19. Shule ya Sekondari ya Mingoyo imetumika kuwakilisha ujenzi wa madarasa yote 56.
Ujenzi wa madarasa hayo umegharimu kiasi cha fedha Bilioni 1,120,000,000/= kwa mchanganuo ufuatao milioni 420 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 21 shule shikizi 8[elimu msingi] na milioni 700 shule za sekondari 14 ujenzi wa madarasa 35 kwa kila darasa shilingi milioni 20,000,000/=.
Mkuu wa mkoa kwa kipekee amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo za ujenzi Mkoani Lindi lakini pia amewashukuru wananchi kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kutekeleza ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa 56 lakini pia kuendelea na moyo huo kwa miradi mingine inayokuja.
Aidha,Mkuu wa Wilaya Ndugu Shaibu Ndemanga alipata wasaa wa kutoa taarifa fupi kwa Wilaya ya Lindi ambapo amesema mpaka kufikia leo ujenzi umekamilika kuna bakaa ya kiasi cha fedha milioni 33,204,982.37/= ambapo kupitia nguvu ya wananchi imeweza kuokoa kiasi hiko cha fedha.
DC ameahidi kuwa wakati mwingine watatumia kiasi kidogo cha fedha kukamilisha miradi, Kwani kupitia miradi hii wamejifunza kuwa inawezekana.
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255717469888
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa