Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia timu ya wataalamu na wajumbe mbalimbali imefanya mdahalo juu ya maswala ya ukatili wa kijinsia hasa mimba za utotoni.Mdahalo huo umefanyika leo tarehe 8/12/2021 katika shule ya msingi Kitomanga,ambapo mwenyekiti wa mdahalo huo alikuwa ni Mhe. Diwani kata ya Kitomanga.
Sababu mbalimbali zimeelezwa ambazo zinachangia ukatili wa kijinsia/mimba za utoto baadhi ya sababu hizo ni pamoja na mmomonyoko wa maadili,wazazi kuozesha watoto wao wakiwa kwenye umri mdogo unyago,umasikini na wazazi kukwepa majukumu.
Mratibu wa Ichf Iliyoboreshwa ndugu Shaibu Mgoba amesema“Sababu kubwa ni baadhi ya wazazi kukwepa majukumu ya kusomesha hivyo kupelekea kuozesha watoto wananapomaliza elimu ya msingi ama kuozesha watoto wakiwa bado wanasoma hivyo kupelekea watoto kupata ujauzito wakiwa kwenye umri mdogo”
Aidha,Gender Champion ndugu Razack Mbaraka ameongeza kuwa jamii kutokuweka kipaumbele katika kulinda haki za mtoto lakini pia watoto kuwa na uhuru kupitiliza ambapo mtoto anaweza kurudi usiku na wazazi wakaona ni kitu cha kawaida.
Katika kutafuta suluhu ya kupinga ukatili wa kijinsia Afisa Lishe wa Manispaa ndugu Mwenda Gella ameshauri suala la kutengeneza mpango mkakati mashuleni,kata,kidini na kuweka ajenda kwenye mikutano kuelimisha watoto na wananchi kwa ujumla juu ya ukatili wa kijinsia na madhara yake.Lakini pia kuhakikisha wazazi wanakuwa mfano wa tabia njema kwa watoto wao ili kuweza kuwafunza maadili mema watoto.
Vilevile Mtendaji wa kata ya Kitomanga amewataka wazazi kutokuwaogopa watoto wao hivyo wakae nao chini na kuwafunza mambo mbalimbali yahusuyo mabadiliko ya kiukuaji(balehe)lakini pia madhara yake na jinsi ya kukwepa vishawishi mbalimbali.
Msaidizi wa polisi dawati la jinsia ametoa rai kwa wananchi kutoa taarifa juu ya ukatili wa kijinsia kwa polisi kata ili kuweza kupata msaada kwa haraka pale unapohitajika kwa masuala ya ukatili wa kijinsia ni kosa la jinai.
Kupitia mdahalo huo mambo mbalimbali yamejadiliwa na suluhu ya kupinga ukatili,ambapo wajumbe wameazimia kutoa elimu kwa jamii juu ya ukatili wa kijinsia na mbinu mbalimbali ambazo zitatumika kupambana na ukatili huo.
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255717469888
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa